Maria De Mattias Secondary School - Items filtered by date: January 2021
Friday, 22 January 2021 07:41

Tangazo la masomo kidato cha tano 2021

SHULE YASEKONDARI YA WASICHANA MARIA DE MATTIAS INAKUTANGAZIA NAFASI ZA MASOMO KWA KIDATO CHA TANO KWA MWAKA WA MASOMO 2021 KWA (TAHASUSI) COMBINATION ZIFUATAZO

CBG, PCB, PCM, PGM, EGM, HGE, ECA, HKL, HGK, HGL

Maria  De Mattias sekondari ni shule  ya Bweni  kwa wasichana  pekee inayomilikiwa na Masista Waabuduo Damu ya Kristo (ASC). Shule ipo umbali wa km6 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma barabara ya Morogoro karibu na stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, Shule ina mazingira Mazuri ya kujifunzia, Maktaba Bora yenye vitabu vyote kwa masomo Yote,Maabara ya kisasa ya Komputa, Walimu wenye sifa Bora na uzoefu wa kufundisha Pia shule ina maabara nzuri kwa masomo ya sayansi.Huduma bora za Bweni, Malezi bora kwa Mwanafunzi yanazingatia Maadili ya kikristo na ya kiafrika.

Sifa za muombaji.

Muombaji awe amefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na daraja la pili katika mitihani yake ya kitaifa ya kidato cha nne na kupata alama  A na B katika tahasusi yake anayotarajia kusoma kidato cha tano na kwa mwanafunzi anayetarajia kusoma miongoni mwa tahasusi hizi za    EGM, PCM, na PGM lazima awe amefaulu somo la hesabu na kupata alama ya C katika somo hilo na tahasusi zingine  kama PCB,  CBG, HGE, ECA, HKL, HGK, HGL  angalau ufaulu wa alama ya D katika somo la hesabu.

  • Fomu ya kujiunga na kidato cha tano zinapatikana shuleni Maria De Mattias au unaweza kupakua fomu hizo katika tovuti ya shule ambayo ni https://mariademattiassec.sc.tz/  au kwa maelekezo zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo. 0679 72 64 61 / 0745 14 15 11 au 0755155140.
  • Usaili (interview) kwa wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano utafanyika tarehe 12/02/2021 hapa shuleni na muda wa kuripoti shuleni  kwa  ajili ya usaili (Interview) utakuwa saa 09:00 kamili asubuhi siku ya Ijumaa.
  • Watakaokuwa wamechaguliwa na shule baada ya usaili watatakiwa kuripoti shuleni 01/03/2021
  • Fomu inapatikana kwa gharama ya Tsh. 25,000 na inalipwa shuleni moja kwa moja.

“Karibu  shule ya Maria De Mattias  kwa Elimu Bora ya mtoto wako.”

 
Published in News
Friday, 22 January 2021 07:33

Sifa za muombaji

15831442411403158700 sifa za muombaji

Published in News

Contact us

Web Traffic

Today
Yesterday
This week
This month
Total139185

Follow us on