Tangazo la Masomo Kidato cha Kwanza 2024

  • 25/08/2023

SHULE YASEKONDARI YA WASICHANA MARIA DE MATTIAS INAKUTANGAZIA NAFASI ZA MASOMO KWA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2024

Maria De Mattias sekondari ni shule ya Bweni  kwa wasichana  pekee inayomilikiwa na Masista Waabuduo Damu ya Kristo (ASC). Shule ipo umbali wa km6 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma barabara ya Morogoro karibu na stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, Shule ina mazingira Mazuri ya kujifunzia, Maktaba Bora yenye vitabu vyote kwa masomo Yote, Maabara ya kisasa ya Komputa, Walimu wenye sifa Bora na uzoefu wa kufundisha Pia shule ina maabara nzuri kwa masomo ya sayansi. Huduma bora za Bweni, Malezi bora kwa Mwanafunzi yanayozingatia Maadili ya kikristo na ya kiafrika.

  • Fomu ya kujiunga na kidato cha kwanza inapatikana shuleni Maria De Mattias au unaweza kupakua fomu hizo katika tovuti ya shule ambayo ni www.mariademattiassec.sc.tz au kwa maelekezo zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo. 0679 72 64 61 / 0745 14 15 11/0756 71 51 73 au 0784 25 02 53.
  • Kwa Wakazi wa Dar es Salaam Fomu za Kujiunga zinapatikana Mbezi Beach Tangi Bovu kwa Masista waabuduo damu ya kristu
  • Fomu inapatikana kwa gharama ya Tsh. 20,000 na inalipwa shuleni moja kwa moja.
  • Mtihani wa Kujiunga Utafanyika tarehe 18/09/2022

"Karibu shule ya Sekondari Maria De Mattias kwa Elimu Bora ya mtoto wako.”

Share

Contact us

Web Traffic

Today
Yesterday
This week
This month
Total139185

Follow us on